FT : Tanzania 2-0 Cape Verde

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Oct 2018
FT : Tanzania 2-0 Cape Verde
Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imefufua matumaini ya kufuzu fainali za michuano ya AFCON 2019 baada ya kuilaza Cape Verde mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa dimba la Taifa jijini Dar es salaam.

Mabadiliko ya kikosi yaliyofanywa na kocha Emmanuel Amunike kwa kuwaanzisha Shomari Kapombe na Kelvin Yondani huku akimtumia kiraka Erasto Nyoni kwenye safu ya kiungo cha chini, yalikuwa na faida kwani yaliimarisha zaidi timu katika kujilinda huku Nyoni akitawala dimba.



Nahodha Mbwana Samatta angeweza kuitanguliza Stars mapema tu kwenye kipindi cha kwanza kama angefunga mkwaju wa penati baada ya Msuva kufanyiwa madhambi kwenye eneo la hatari.

Hata hivyo kwenye dakika ya 29 Samatta alisahihisha makosa yake baada ya kuwaramba chenga walinzi wa Cape Verde kabla ya kumtengea pasi murua Simon Msuva aliyeihesabia Stars bao la kuongoza.



Samatta aliyekuwa mwiba mkali kwa safu ya ulinzi ya Cape Verde aliifungia Stars bao la pili kwenye dakika ya 65 baada ya kuachia shuti kali akiwa ndani ya 18.

Samatta alianzisha shambulizi lililozaa bao hilo ambapo alipasiana na Mudathir Yahya kabla ya kurejeshewa mpira huo na kuujaza kambani.



Licha ya kumiliki mpira kwa muda mwingi, Cape Verde ilishindwa kuipenya ngome ya Stars iliyotumia mfumo wa kujilinda na kushambulia kwa pamoja.

Ushindi huo umeipandisha Stars hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi L baada ya kufikisha alama tano.

Kama Uganda itaifunga Lesotho au hata matokeo ya sare, yatatosha kuibakisha Stars kwenye nafasi ya pili baada ya mzunguuko wa nne.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’