Hans Poppe afikishwa Mahakama ya Kisutu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Oct 2018
Hans Poppe afikishwa Mahakama ya Kisutu
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe amefikishwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu kesi inayomkabili ya madai ya kutoa taarifa za uongo kuhusiana na malipo ya kodi, kifungu 106(1) A& C (i) cha Income Tax Act sura ya 332 R.F 2008, kati ya Machi 10, 2016 na Septemba 30, 2016.

Hans Poppe na mfanyabiashara, Franklin Lauwo wamefikishwa katika Mahakama hiyo, saa tatu na nusu na kupelekwa moja kwa moja katika chumba cha mahabusu wakisubiri kupandishwa kizimbani.

Aprili 30, 2018, mahakama hiyo iliamuru washtakiwa Hanspoppe na Lauwo wakamatwe popote walipo.

Mahakama hiyo ilitoa amri hiyo baada ya upande wa mashtaka kupitia kwa Wakili Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Leonard Swai kuieleza kuwa wamewatafuta washtakiwa hao tangu Machi 16 mwaka huu bila mafanikio

Hanspope na Lauwo wameletwa na Gari ya Takukuru na bado hawajapandishwa kizimbani mpaka sasa.

Hans Poppe alikamatwa juzi Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati akirejea nchini.

Hans Poppe leo Jumanne anaunganishwa kwenye kesi inayowakabili Rais wa Simba, Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange 'Kaburu'.

Septemba 14 mwaka huu, Takukuru ilitangaza kuwasaka Hans Poppe na mkandarasi Franklin Peter Lauwo ili kuunganishwa katika kesi ya utakatishaji fedha inayowashilishilia kina Aveva.

Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali John Mbungo alithibitisha juu ya jambo hilo na mchakato mzima ulivyokuwa.

"Nikweli tumefanikiwa kumnasa Hans Poppe, kama nilivyowaekeza awali tulikuwa tunamtafuta sasa jana (juzi) tulipata taarifa anakuja nchini," alisema Mbungo.

"Tukajiweka sawa kwa kuweka mtego na maafisa wetu wakafanikiwa kumnasa na mpaka sasa tunaye tukiendelea na majukumu yetu ya kikazi.

"Kitakachofuata baada ya hapa nafikiri kesho (leo) Jumanne tutampandisha mahakamani kuendelea na kesi inayomkabili itategemea mahakama itaamua nini, ila hicho ndicho kitakachoendelea."

Watuhumiwa hao walikuwa wakisakwa ili kuunganishwa kwenye kesi inayowakabili kina Aveva iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu yenye mashtaka kumi likiwemo la kula njama, matumizi mabaya na kughushi nyaraka ikionyesha Klabu ya Simba inalipa mkopo wa Dola za Marekani 300,000 kwa Aveva kitu ambacho si kweli.

Wanadaiwa kuwa, Machi 10 na 16, 2016, Aveva na Nyange waliandaa nyaraka za kuhamisha dola za kimarekani 300,000 kutoka kwenye akaunti ya klabu ya Simba kwenda kwenye akaunti ya Aveva wakijua kuwa wanachofanya ni kosa.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
6h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
6h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
9h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’