Stars yasaka ushindi muhimu uwanja wa Taifa leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Oct 2018
Stars yasaka ushindi muhimu uwanja wa Taifa leo
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo kinashuka kwenye uwanja wa Taifa kuikabili Cape Verde katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za michuano ya AFCON 2019.

Stars inashika nafasi ya nne kundi L ikiwa na alama mbili lakini ushindi katika mchezo wa leo unaweza kuipeleka hadi nafasi ya pili kutegemeana na matokeo ya mchezo kati ya Lesotho dhidi ya Uganda.

Ukiiacha Uganda ambayo iko katika nafasi nzuri zaidi ya kufuzu, Cape Verde, Tanzania na Lesotho zina nafasi sawa kimahesabu katika kuwania nafasi nyingine iliyobaki.

Timu mbili kutoka kila kundi zitafuzu kwa fainali za AFCON 2019 zitakazofanyika mwezi Juni nchini Cameroon baada ya CAF kuongeza idadi ya timu kutoka 16 hadi 24.

Baada ya mchezo wa leo, Stars itakuwa na mchezo mwingine ugenini dhidi ya Lesotho mwezi ujao.

Ushindi katika mchezo wa leo na ushindi katika mchezo mwingine wa nyumbani dhidi ya Uganda ni matokeo ambayo yataiweka Stars katika nafasi nzuri ya kufuzu

Matokeo tofauti na ushindi kwenye mchezo wa leo yatafifisha matumaini ya kufuzu kwa michuano hiyo ambayo Tanzania ilishiriki kwa mara ya mwisho miaka 38 iliyopita.

Watanzania wameaswa kujitokeza kwa wingi uwanja wa Taifa leo katika mchezo huo unaotarajiwa kuanza saa 11 jioni.

Viingilio vya mchezo huo ni Tsh 2,000/- Mzunguuko wakati Majukwaa yote ya VIP ni Tsh 10,000/-
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
13h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
19h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
21h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’