Poppe arejea, akamatwa na TAKUKURU

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Oct 2018
Poppe arejea, akamatwa na TAKUKURU
Mwezi uliopita Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ilitangaza kumtafuta Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba Zacharia Hans Poppe.

Poppe amekamatwa na TAKUKURU jana kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam (JNIA) wakati akitokea Marekani.

Atajumuishwa kwenye kesi ya utakatishaji fedha na kughushi inayowakabili Rais wa Simba Evans Aveva na Makamu wake Geofrey Nyange Kaburu.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na ndugu zake, Poppe alikuwa nchini Marekani akitibiwa majeraha ya mguu.

Amerejea jana baada ya kumaliza matibabu hayo.

Taarifa zaidi imebainisha kuwa kiongozi huyo amerejea mapema ili kuharakisha usikilizwaji wa kesi inayowakabili viongozi wakuu wa Simba ambao wamekuwa mahabusu tangu mwaka uliopita.

"Hans Poppe amerejea mwenyewe, alifanya hivyo baada ya kumaliza matibabu, lakini aliona huruma kwa kuwa Aveva ni mgonjwa, akasema angependa kurejea haraka kama anakamatwa sawa lakini ajumuishwe na kesi iendelee."
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’