Familia ya Mfanyabiashara Mohammed Dewji 'MO' ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya METL, imeahidi donge nono la fedha taslimu kiasi cha Tsh Bilioni moja kwa mtu atakayetoa taarifa zitakazofanikisha kupatikana kwa mtoto wao aliyetekwa Alhamisi iliyopita.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Msemaji wa familia Azim Dewji amesema mtoa taarifa huyo atalindwa.
Aidha Dewji ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada inazofanya katika kuwatafuta wahalifu waliomteka MO.
Azim amevishukuru vyombo vya habari kwa kuuhabarisha UMMA kuhusiana na tukio hilo na amevitaka viendee kutoa taarifa.
Ametoa shukrani za kipekee kwa taasisi za dini ambazo zimekuwa zikiendesha maombi kwa ajili ya MO ili aweze kupatikana akiwa salama.
Dewji ametoa namba za mawasiliano ambazo zinaweza kutumiwa na yeyote mwenye taarifa sahihi zitakazofanikisha kupatikana kwa MO.
Kwa yeyote mwenye taarifa awasiliane na;
MURTAZA DEWJI
0755030014
0717208478
0784783228

ADVERTISE HERE