Mchakato wa uchaguzi Simba unaendelea

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
15 Oct 2018
Mchakato wa uchaguzi Simba unaendelea
Leo Jumatatu ni siku ya nne ambazo ni zaidi ya saa 96 tangu tukio la kutekwa kwa Bilionea, Mohammed ‘MO’ Dewji katika hoteli ya Collosseum na kuleta taharuki kubwa nchini juu ya usalama wake.

Hata hivyo, licha ya Wana Msimbazi wakiwa bado wapo njia panda juu ya hatma ya mfadhili na mdhamini wao huyo, mambo mengi klabuni yanaendelea ikiwamo mchakato wa Uchaguzi Mkuu.

Awali kulikuwa na hofu kwamba tukio la kutekwa kwa Mo Dewji kungeathiri mchakato wa uchaguzi huo, lakini jana Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Boniphace Lyamwike, alisisitiza uchaguzi upo.

Akizungumza na Mwanaspoti, Lyamwike alisema viongozi wengi na wadau wengi wa klabu yao wamekuwa na maswali mengi kuhusu uchaguzi huo, lakini ukweli hakuna mabadilikop yoyote juu yake.

“Simba ni taasisi, uchaguzi hauwezi kusimama na mambo mengine yataendelea polepole kama tulipanga na watu wanabidi wafahamu hivyo,” alisema Lyamwike.

Alisema leo Jumatatu watafanya kikao cha kamati ili kutangaza tarehe rasmi ya wagombea kuanza kampeni ili kujinadi kabla ya uchaguzi utaofanyika siku moja na Mkutano Mkuu wa klabu hiyo.

“Kesho (leo) jioni tutakutana ili kupanga na kutangaza tarehe ya kuanza kufanya kampeni,” alisema.

MO Dewji, alitekwa alfajiri ya Alhamisi iliyopita alipoenda hoteli ya Colosseum yenye kituo cha mazoezi (gym) na watu wawili wanatajwa kuwa wazungu na kutofahamika mahali alipo hadi sasa.

Tangu kutowekwa kwa MO Dewji, kuanzia viongozi, wachezaji, wanachama na mashabiki wa klabu hiyo wamekuwa wakimuomboleza wengine wakiendesha dua maalumu ili kumuombea kwa Mungu amnusuru huko alipo, ikiwezekana arejee salama akiwa mzima wa afya aendelee na majukumu yake ya kawaida.

Serikali juzi kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola alisema bado wanaendelea kumsaka bilionea huyo sambamba na polisi kuwasaka watuhumiwa walioshiriki tukio hilo, huku akisema wanaoshikiliwa walikuwa watu 26 akiwamo Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →