Uwanja wa Taifa kufunguliwa Novemba 24

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Nov 2017
Uwanja wa Taifa kufunguliwa Novemba 24
Uwanja mkuu wa Taifa ambao ulikuwa katika matengenezo kwa takribani miezi mitatu, uko tayari kuanza kutumika Novemba 24 mwaka huu.

Akizungumza wakati wa kukabidhiwa Uwanja huo jana, Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, amesema kwamba, Uwanja ni mzuri na sasa unaonekana kukamilika kwani hata vile vipara vilivyokuwa vinaonekana awali vimepotea.

Mwakyembe alisema, Serikali itakabidhiwa Uwanja huo rasmi na Kampuni ya SportPesa ndani ya siku 10 na hivyo kuiomba TFF kwa kushirikiana na bodi ya Ligi kupanga mechi moja ichezwe katika zoezi la uzinduzi na makabidhiano ya uwanja huo.

Ò€œUwanja umekamilika na leo(jana) nimeukagua na kuridhishwa na ukarabati mkubwa uliofanywa, wamenambia baada ya siku 10 utakuwa tayari hivyo nimewaomba TFF kuangalia uwezekano wa kutafuta japo mechi moja ichezwe wakati wa ufunguzi Novemba 24,Ò€ alisema Mwakyembe.

Aliongeza kuwa wapo vijana sita ambao wamepatiwa mafunzo ya utengenezaji wa Uwanja hivyo ameomba kuangaliwa kwa ajira zao ili waweze kutumika katika viwanja vingine vya mikoani.

Mwakyembe alisema, kubwa linalotakiwa kwa sasa ni watanzani kwa ujumla kushirikiana katika kuutunza uwanja huo kwani gharama kubwa zimetumika katika ukarabati wake ambazo awali zilitajwa ni shilingi Bilioni 1.2 lakini ukimalizika kabisa ndiyo watajua gharama zote zilizotumika.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’