Omog aachwe afanye kazi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Sep 2017
Omog aachwe afanye kazi
Kumekuwa na shinikizo kubwa kutoka kwa baadhi ya mashabiki wa Simba wakitaka mabadiliko kwenye benchi la Ufundi, ambapo wengi wanataka kocha Joseph Omog afungashiwe virago.

Omog aliyeanza kuifundisha Simba msimu uliopita aliiwezesha kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi sambamba na kutwaa kombe la FA (ASFC) na hivyo kuiwezesha Simba kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la shirikisho msimu huu.

Huu ni msimu wake wa pili akiwa na kikosi kinachoaminika kuwa bora zaidi kwenye ligi kuu ya Vodacom msimu huu.

Mpaka sasa hajafanya vibaya kwani Simba iko nafasi ya nne ikiwa na alama nane na mabao 10. Imepitwa alama mbili tu na vinara wa ligi Mtibwa Sugar wenye alama 10.

Hakuna shaka kuwa lengo namba moja la benchi la ufundi msimu huu ni kutwaa ubingwa wa ligi kuu kuondoa nuksi ya kulikosa kombe hilo misimu mitano iliyopita.

Simba ina uwezo wa kutwaa taji chini ya Omog. Nasisitiza uwezo huo upo chini ya Omog. Muhimu ni kumuunga mkono tu.

Tukumbuke Simba imefanya usajili wa karibu kikosi kizima. Kwa kocha yeyote sio rahisi kutengeneza timu imara kwa siku moja baada ya mabadiliko ya wachezaji wengi.

Hili lilizungumzwa hata kabla ligi haijaanza. Kwamba licha ya kusajili kikosi bora kabisa, bado kocha atahitaji muda kutengeneza muunganiko mzuri wa timu.

Omog bado hajapata kikosi chake bora kwenye baadhi ya maeneo ndio maana amekuwa akibadili mfumo katika karibu kila mchezo.

Atafanikiwa, wala tusiwe na wasiwasi. Mapungufu ya Simba yapo kwenye safu ya ushambuliaji tu na hili limekuwa likifanyiwa kazi.

Simba ndiyo timu inayocheza 'sexy football' hakuna zaidi yake hapa Tanzania. Ni burudani kuiangalia Simba ikicheza.

Tusiwe kama wenzetu wa upande ule ambao wanapiga kelele kocha wao afukuzwe kwa kuwa timu yao haichezi vizuri kabisa.

Sisi tuna timu bora kila mmoja anafahamu, muhimu tuliache benchi la ufundi lirekebishe mapungufu yaliyojitokeza.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’