Saa 87 za MO Dewji

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
15 Oct 2018
Saa 87 za MO Dewji
Zikiwa zimepita saa 87 tangu kutekwa mfanyabiashara Mohammed Dewji ‘Mo’, serikali imesema itavisimamia vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha inawakamata na kuwatia nguvuni watu wanaohusika na matukio ya utekaji wa raia.

Mo (43), alitekwa Alhamisi saa 11 alfajiri na watu wasiojulikana katika Hoteli ya Colosseum iliyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam alikokwenda kwa ajili ya kufanya mazoezi kwenye gym ya hoteli hiyo.

Hadi jana saa 2:00 mfanyabiashara huyo alikuwa hajapatikana ikiwa ni saa 87 tangu kutekwa kwake.

Akizungumza na Nipashe kwa simu jana, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema hajapata taarifa zozote za kushikiriwa kwa watuhumiwa zaidi kuhusiana na tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara huyo.

Mambosasa alisema kuwa kwa siku ya jana vijana wake hawajampelekea taarifa yoyote mpya juu ya tukio hilo.

Wakati Kamanda Mambosasa akiyasema hayo, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jana ilisema itavisimamia vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha inawakamata na kuwatia nguvuni watu wanaohusika na matukio ya utekaji wa raia.

Naibu Waziri wa wizara hiyo, Hamad Yusuf Masauni, alisema hayo jana alipokuwa akizungumza na wananchi wa Kata ya Murieti, nje kidogo ya Jiji la Arusha katika ziara yake ya kikazi.

Alisema kumekuwapo kwa taarifa za upotoshaji katika jambo la utekwaji wa watu ambapo baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakivishtumu vyombo vya usalama kuwa havichukui hatua za kudhibiti matukio hayo.

"Kwanza, nimpongeze Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, kwa jitihada zake za dhati za kupambana na uhalifu wa utekwaji wa watu na juzi alizungumza na vyombo vya habari na alilifafanua vizuri jambo hili na jitihada za serikali katika kukabiliana na matukio ya utekaji wa watu hapa nchi," alisema.

Naibu waziri aliongeza kuwa kupitia Jeshi la Polisi, watakabiliana na matatizo ya uhalifu likiwamo la matukio ya utekaji ambayo yameshika kasi nchini.

"Siku chache zilizopita, mfanyabiashara maarufu hapa nchini, Mohamed Dewji alitekwa na watu wasiyojulikana. Kutokana na umaarufu wake tukio hilo limechukua hisia kubwa ndani ya nchi na nje na ndiyo sababu Waziri Lugola alizungumzia tukio hilo na kutoa takwimu za matukio ya utekaji," alisema Masauni.

Kiongozi huyo wa serikali alisema wananchi wamekuwa na hisia na hofu kuhusiana na matukio hayo, lakini akawataka kuwa wavumilivu kwa kuwa serikali imejipanga kukabiliana na wahalifu wanaofanya matukio hayo.

"Serikali inathamini maisha ya kila raia na matukio hayo yanaendelea kufanyiwa upelelezi na watuhumiwa wanakamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria," Masauni alisema na kuongeza:

"Tutalisimamia Jeshi la Polisi huhakikisha wanazidisha nguvu kuwatafuta hawa watu wasiojulikana ili sasa wajulikane.”

Licha ya kuzungumza hayo, alisema kuwa serikali inatambua changamoto ya mazingira ambayo yanalikabili jeshi hilo ambayo wakati mwingine yanachelewesha utendaji wa kazi zake.

“Katika Mkoa wa Arusha, kwa mfano, ni mkoa wa kimkakati unaojihusisha na mambo ya utalii [ambao] unachangia asilimia kubwa ya uchumi wetu lakini unakabiliwa na changamoto ya mipaka mingi na yenye vipenyo vingi, hivyo masuala ya uhalifu yanaweza kufanyika kwenye maeneo hayo," alisema.

Alieleza kuwa serikali imejipanga kutumia sayansi na teknolojia katika kuthibiti mipaka yote nchini na kuwabaini wahalifu kwa kutumia vifaa vya teknolojia ya kisasa zikiwamo kamera za CCTV ambazo zitafungwa kwenye miji mikuu yote nchini.

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Arusha, Jonas Kore, alimwomba kiongozi huyo wa serikali kuhakikisha ulinzi na usalama kwa raia na mali zao unaimarishwa.

Mwananchi huyo pia aliiomba wizara hiyo kuhakikisha inalisimamia Jeshi la Polisi kutoa dhamana kwa wakati kwa raia

Nipashe
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
16m ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →