Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Emmanuel Amunike amemuongeza beki kiraka wa Simba Erasto Nyoni kwenye kikosi chake kinachotarajiwa kuivaa Cape Verde keshokutwa.
Udhaifu ulioonyeshwa na safu ya ulinzi ya Stars kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Cape Verde ambapo Stars ililazwa mabao 3-0, umepelekea wadau wa soka nchini kupaza sauti kumtaka kocha huyo amuongeze Nyoni kutokana na uzoefu wake wa kushiriki michezo mingi ya Kimataifa.
Stars inatarajiwa kuivaa Cape Verde Jumanne katika dimba la Taifa kwenye mchezo wa kusaka tiketi ya kufuzu fainali za AFCON 2019.
Stars inahitaji kushinda mchezo huo ili kuweka hai matumaini ya kufuzu kwa fainali za michuano hiyo.
Tayari shirikisho la soka Tanzania (TFF) limetaja viingilio vya mchezo huo unaotarajiwa kupigwa keshokutwa saa 11 jioni ambapo kiingilio cha chini kabisa ni Tsh 2,000/-

ADVERTISE HERE