Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' imerejea jana kutoka visiwa vya Cape Verde na ina siku mbili za kujiandaa na mchezo mwingine wa kufuzu kwa fainali za AFCON 2019 dhidi ya Cape Verde.
Mchezo huo utapigwa keshokutwa Jumanne, Oktoba 16 kwenye dimba la Taifa.
Baada ya kipigo cha mabao 3-0 juzi, Stars ni lazima iibuke na ushindi kwenye mchezo huo ili kuweka hai matumaini ya kufuzu.
Kocha Msaidizi wa Stars Hamedi Morocco amesema watayafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo wa juzi ili waweze kuibuka na ushindi nyumbani.
Morocco amewataka Watanzania wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa keshokutwa ili kuipa sapoti timu yao iweze kuibuka na ushindi.
"Cape Verde walipata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wao. Uwanja wao unachukua watu 15,000 tu sisi uwanja wetu unachukua watu 60,000"
"Kama watu 60,000 wataingia uwanjani keshokutwa, mazingira hayo yataongeza morali kwa wachezaji na hakuna litakaloshindikana kupata ushindi."

ADVERTISE HERE