Wanaoshikiliwa kutekwa kwa MO wafika 20

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Oct 2018
Wanaoshikiliwa kutekwa kwa MO wafika 20
Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema kwamba watu 20 wanashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini hadi sasa kwa ajili ya uchunguzi juu ya kutekwa kwa Mfanyabiashara Bilionea, Mohammed β€˜Mo’ Dewji juzi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Lugola amesema kwamba Jeshi la Polisi nchini linaendelea kumtafuta mfayabiashara huyo likiwa na imani kubwa ya kumpata akiwa salama.

Waziri Lugola amelitaka jeshi la Polisi kuharakisha upelelezi wake ili lisiwashikilie washukiwa kwa zaidi ya saa 24.

Aidha, Waziri Lugola amewataka wananchi kutoa taarifa zitakazoweza kulisaidia Jeshi la Polisi kupatikana kwa Mohammed Dewji.

"Sababu za matukio ya kutekwa yanayotokea ni pamoja na kisiasa, kiuchumi, kimapenzi na njaa ili mtu apate fedha na sababu za kutekwa kwa Mohamed Dewji zitajulika hapo wahalifu watakapojulikana," amesema Lugola.

Dewji mwenye umri wa miaka 43 alitekwa juzi asubuhi akiwa anaingia katika gym ya Collessium eneo la Masaki mjini Dar es Salaam kufanya mazoezi baada ya watu wasiojulikana kufyatua risasi hewani mfululizo wakati bilionea huyo anateremka kwenye gari yake kabla ya kumbeba na kumpakia kwenye gari lao na kutokomea naye kusikojulikana
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’