Mshambuliaji wa Kimataifa wa Simba Emmanuel Okwi leo ameiongoza timu yake ya Taifa ya Uganda kuondoka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Lesotho katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019.
Okwi aliibuka nyota wa mchezo huo baada ya kufunga mabao mawili huku akisababisha penati ya bao lililofungwa na Faruq Miya.
Ushindi huo umeirudisha Uganda kileleni mwa kundi L baada ya kufikisha alama saba.
Cape Verde iliyoifunga Tanzania 3-0 jana imeshushwa nafasi ya pili ikiwa na alama nne.
Lesotho na Tanzania zinaendelea kufuatana mkiani zote zikiwa na alama mbili na pia zimepoteza michezo ya mzunguuko wa tatu kwa idadi sawa ya mabao.

ADVERTISE HERE