Kulingana na taarifa zilizotolewa na Jeshi la Polisi jana jioni, watu 12 wanashikiliwa kutokana na tukio la utekaji wa Mfanyabiashara maarufu nchini Mohammed Dewji 'MO' ambaye pia ni mwekezaji wa klabu ya Simba.
Imeingia siku ya pili leo tangu tajiri huyo mashuhuri nchini Tanzania na Afrika kwa ujumla atekwe nyara na watu wasiojulikana.
Mo alitekwa jana alfajiri wakati akielekea katika ukumbi wa mazoezi katika hoteli moja ya kifahari jijini Dar es Salaam.
Leo Ijumaa Jeshi la Polisi linatarajiwa kutoa taarifa kwa UMMA wa Watanzania na dunia kwa ujumla juu ya mwendelezo wa uchunguzi wa tukio hilo.
Bado haijafahamika ni akina nani wamehusika na uhalifu huo licha ya mamlaka kusema kulikuwa na wazungu wawili walioshiriki.
Mo, mwenye miaka 43, anakisiwa na jarida la masuala ya kifedha la Forbes kuwa na utajiri wa dola bilioni 1.5 kiasi kinachomfanya kuwa tajiri namba moja Afrika Mashariki na tajiri mwenye umri mdogo zaidi Afrika nzima.

ADVERTISE HERE