MO aitikisa dunia, ajadiliwa kila mahali

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Oct 2018
MO aitikisa dunia, ajadiliwa kila mahali
Kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu ambaye ndiye bosi mkuu wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji, kumetikisha, si tu Tanzania bali hata anga za kimataifa.

Jarida la Forbes ambalo limekuwa likifanya utafiti wake na kumtangaza mara kwa mara Dewji kama mfanyabiashara kijana aliyefanikiwa zaidi, limeandika habari zake.

Forbes lilisema kuwa Dewji anashika nafasi ya 17 kwa utajiri unaofikia Dola 1.5 bilioni.

Vyombo vya habari vya Uingereza, ikiwemo Shirika la Utangazaji, (BBC), Shirika la Habari la Uingereza (Reuters) na baadhi ya magazeti ya; The times, Daily Telegraph, Daily Mail, Irish Times, The Guardian na The Independent yameandika habari za Dewji.

Pia habari za Dewji zimetua Canada ikiwemo gazeti la Ottawacitizen , Voice of America, Sauti ya Ujerumani na Voice of America (VOA).

Kituo cha habari maarufu cha Marekani, CNN kimerusha habari za Dewji pamoja na kituo cha televisheni cha Al Jazeera cha Qatar kimeandika habari za mfanyabiashara huyo.

Dewji inaelezwa ni kati ya wawekezaji wazawa wenye sifa za kutengeneza ajira zaidi ya 20,000 Tanzania na amekuwa akiendesha biashara zake Afrika Mashariki na Kati.

Kupitia Kampuni yake ya METL Group, ameweza kumiliki viwanda zaidi ya 35 katika masuala mbalimbali ikiwemo; kilimo, uzalishaji mali, masuala ya nishati ya gesi na petroli, huduma za fedha, simu za mkononi, mashamba na maeneo ya makazi, usafirishaji, na usambazaji.

Jeshi la Polisi linaendelea na msako wa wahalifu waliomteka
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
29m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’