Kesho Ijumaa saa mbili usiku kwa saa za Tanzania, kikosi cha timu yetu ya Taifa 'Taifa Stars' kitakuwa uwanjani huko Cape Verde kupepetana na wenyeji wao katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za michuano ya AFCON 2019.
Stars iko Cape Verde tangu mapema jana ambapo siku hiyo jioni ilipata nafasi ya kujifua kwenye uwanja wa Estadio Nacional De Cabo Verde kujiandaa na mchezo huo.
Stars inashika nafasi ya tatu kundi L ikiwa imejikusanyia alama mbili baada ya kutoka sare katika michezo yake miwili ya kwanza.
Uganda inaongoza kundi L ikiwa na alama nne ikifuatiwa na Lesotho iliyo na alama mbili sawa na Stars.
Cape Verde inaburuza mkia katika kundi hilo ikiwa na alama moja.
Ushindi au hata sare kwenye mchezo wa kesho utaisaidia Stars kujiweka katika nafasi nzuri kabla ya mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumanne ijayo kwenye uwanja wa Taifa.
Kocha Mkuu wa Stars Emmanuel Amunike amewahakikishia Watanzania kuwa wamejiandaa kikamilifu kupata matokeo chanya kwenye mchezo huo.
Stars inasaka nafasi ya kutinga fainali za AFCON kwa mara ya pili katika historia yake ikiwa imefuzu kwa mara ya mwisho mwaka 1980.
Baada ya mchezo wa kesho Stars itakuwa imebakisha michezo mitatu, miwili ikitarajiwa kupigwa Tanzania.
Hivyo kama itafanya vizuri kwenye mchezo wa kesho, halafu ikashinda michezo yote miwili ya nyumbani, Stars inaweza kurudia kile ilichofanya mwaka 1980.

ADVERTISE HERE