Kumekuwa na mkanganyiko mkubwa juu ya kutekwa kwa Mfanyabishara na Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji.
Muda mchache uliopita mitandao ya Mwananchi na MillardAyo iliripoti kupatikana kwa MO kulingana na taarifa walizozipata kutoka kwa Mkuu wa mkoa na RPC.
Hata hivyo Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda amekanusha kutoa taarifa hiyo na kusisitiza bado MO hajapatikana na wanaendelea kuwasaka waliohusika na tukio hilo.
Makonda amesema msako mkali unaendelea kuwatia nguvuni wote waliohusika katika utekaji huyo.
Watuhumiwa watatu tayari wamekamatwa.
"Mpaka sasa Jeshi la polisi limekamata watu watatu waliohusika katika utekaji wa bilionea Mohamed 'Mo' Dewji. Tutahakikisha Mo tunampata akiwa salama," amesema

ADVERTISE HERE