Ndanda Fc yakwama Singida, yaomba ichangiwe na wadau

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Oct 2018
Ndanda Fc yakwama Singida, yaomba ichangiwe na wadau
Utaratibu mpya wa mapato yote ya mlangoni kuchukuliwa na timu mwenyeji ni kama umeanza kuzigharimu baadhi ya timu za ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya klabu ya Ndanda Fc kukwama mkoani Singida baada ya kuishiwa fedha.

Afisa habari wa Ndanda FC Idrisa Bandari amethibitisha taarifa ya timu hiyo kushindwa kusafiri kutoka Singida kurudi Mtwara kutokana na kukosa fedha.

"Ni kweli, tulikuwa na safari ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya mechi zetu tatu. Mechi ya tatu ilikuwa pale Singida dhidi ya Singida United tukafungwa, baada ya hapo kiutaratibu timu ilitakiwa kuondoka kurejea Mtwara kwa sababu kuna mechi mbili (dhidi ya Mbeya City na Biashara)," amesema

"Kwa hiyo kwa utaratibu wa kawaida lazima timu irejee lakini kumekuwa na tatizo kubwa hasa sehemu ya malazi, chakula na fedha ya mafuta kuwasaidia kufika Mtwara."

"Kwa haraka mpaka siku ya jana, tulikuwa tunadaiwa shilingi milioni 3.5 ambazo ni lazima zipatikane zilipwe ndipo timu iweze kurudi Mtwara. Jitihada kubwa sana zilifanyika na mwisho kabisa ilikuwa ni kwenda kukopa fedha kwenye bodi ya ligi ambayo inasimamia michezo ya ligi kuu Tanzania bara na wao wakatuahidi Jumatatu tungekopeshwa fedha ambayo ingekatwa kutoka kwenye mapato yetu yatokanayo na udhamini wa kawaida."

"Ilipofika Jumatatu jioni tukapata taarifa ya maandishi kwamba matarajio yao ya kutukopesha fedha ambazo zingesaidia timu kutoka Singida kurudi Mtwara yameshindikana kwa hiyo tutafute namna nyingine itakayotusaidia kuisafirisha timu.

"Hadi tunavyozungumza mambo yanazidi kuwa magumu zaidi, tumewasiliana na RC amesema matatizo yetu ameyasikia na anajaribu kuona namna ya kusaidia kuhakikisha timu inasafiri kurejea Mtwara."

"Kama viongozi hatupendi kufika huko lakini hali ya kiuchumi si njema na gharama zimekuwa kubwa za kuiendesha timu kwa hiyo mazingira yamekuwa hivyo, sasa ni jukumu la wadau na watu tofauti wanaoipenda klabu kuchangia kwa sababu ni timu ya wanamtwara wote"

Kuanza kujitokeza kwa matukio haya mapema ni dalili mbaya kwa mustakabali wa ligi kuu ya Tanzania Bara.

Kwa kuwa ligi imekosa udhamini basi ni vyema ule utaratibu wa zamani wa kugawana mapato kwenye kila mchezo ukazingatiwa.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
43m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’