Ndio nimeuwasha moto sasa - Kichuya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Oct 2018
Ndio nimeuwasha moto sasa - Kichuya
Mshambuliaji wa Simba,Shiza Kichuya amesema bao lake la kwanza lilofunga msimu huu dhdi ya African Lyon litamfungulia njia ya kufunga mengine zaidi.

Kichuya ameanza msimu vibaya huku akionekana kushuka kiwango jambo lililosababisha akachwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania'Taifa Stars.

Kichuya alisema alikuwa akitafuta sana nafasi ya kufunga ili apate morali ya kufanya vizuri zaidi na anashukuru ametimiza jambo hilo Oktoba 6 mwaka huu alipofunga bao moja katika ushindi ya mabao 2-1 ilioupata Simba dhidi ya African Lyon.

"Kufunga inategemea na nafasi unayopata lakini wengi hawajui kuwa wakati mwingine kocha ananipa majukumu tofauti hivyo nakuwa sina nafasi kubwa ya kufunga kama wengi wanavyotaka.

"Nafurahi nimefunga bao langu la kwanza msimu huu na naamini bao hilo litanipa morali ya kuendelea kufunga zaidi pale nitakapopata nafasi ya kufanya hivyo.

Kichuya alisema ligi ya msimu huu ni ngumu lakini anaamini watatetea ubingwa wao licha ya kwamba wako nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi.

"Ligi imekuwa ngumu msimu huu lakini nafasi ya kutetea ubingwa wetu ipo tena kubwa muhimu ni kila mchezaji kuongeza juhudi na kutimiza majukumu yake ipasavyo"alisema Kichuya.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
2h ago
READ MORE β†’
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
2h ago
READ MORE β†’
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
6h ago
READ MORE β†’
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
8h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
1d ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
1d ago
READ MORE β†’