Mkude yuko vizuri, arejea kambi ya timu ya Taifa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Oct 2018
Mkude yuko vizuri, arejea kambi ya timu ya Taifa
Juzi kiungo fundi wa Simba Jonas Mkude aliwatia hofu mashabiki wa timu hiyo baada ya kupata majeraha kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara dhidi ya African Lyon.

Hofu hiyo haikuwa kwa mashabiki wa Simba tu, bali hata kwa mashabiki wa soka nchini kwani Mkude ni miongoni mwa wachezaji wanaotegemewa kuibeba Stars kwenye michezo ya kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019 dhidi ya Cape Verde.

Habari njema ni kwamba Mkude alipata majeraha ya kawaida kwenye mchezo huo na tayari amerejea kambi ya timu ya Taifa.

Mbali na Mkude wachezaji wengine wa Simba ambao tayari wamerejea kambi ya timu ya Taifa ni Aishi Manula na Shomari Kapombe.

John Bocco hakuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichocheza na African Lyon kutokana anatumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu.

Nahodha huyo wa Simba alibaki kambini akiendelea kujifua kwenye kikosi cha Stars kinachonolewa na nyota wa zamani wa Nigeria, Emmanuel Amunike.

Haruna Niyonzima na Meddie Kagere wao wameondoka kwenda kujinga na kambi ya timu ya Taifa ya Rwanda, Okwi na Murshidi timu ya Taifa ya Uganda na Cleotus Chama timu ya Taifa ya Zambia
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’