Upumzike kwa Amani Mzee Ahmed Jongo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
8 Oct 2018
Upumzike kwa Amani Mzee Ahmed Jongo
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya mtangazaji wa zamani wa michezo Ahmed Jongo aliyefariki jana hospitali ya Temeke mjini Dar es Salaam.

Jongo alistaafu utangazaji wa Redio Tanzania, kwa sasa TBC 2005 na kwa muda sasa amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya kiafya.

Kwa mujibu wa familia ya marehemu, mwili wa Jongo unatarajiwa kupumzishwa leo Saa 7:00 mchana katika makaburi ya Tandika mjini Dar es Salaam.

Na kwa niaba ya TFF, Karia ametoa pole kwa wafiwa, familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huo.

“Nimepokea kwa majonzi makubwa taarifa ya kifo cha Ahmed Jongo,kwa niaba ya TFF natoa pole kwa ndugu,jamaa na marafiki,hakika tutamkumbuka kwa umahiri wake wa kutangaza mpira wa miguu”.

Rais wa TFF, Karia amesema Jongo enzi za uhai wake alipokuwa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD) alikuwa chachu ya Watanzania wengi kufuatilia mpira wa miguu kutokana na umahiri wake wa kutangaza mpira kupitia matangazo ya moja kwa moja kwenye Radio.

Amesema aina ya utangazaji wa mpira wa Jongo ulishawishi wengi kufuatilia mpira wa miguu na kuhudhuria kutazama mechi mbalimbali.

Jongo ametangaza mechi nyingi akiwa RTD, lakini mchezo maarufu zaidi ni wa marudiano kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 1979 mjini Ndola, baina ya wenyeji Zambia na Tanzania.

"Tunakwenda Lagos...Tunakwenda Lagos...Tunakwenda Lagos" ilikuwa ni sauti ya Jongo baadaya filimbi ya mwisho kuwaarifu Watazania kupitia RTD baada ya filimbi ya mwisho Taifa Stars ikitoa sare ya 1-1 na KK 11 na kufuzu CAN (sasa AFCON) kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam.

Shujaa wa Tanzania siku hiyo alikuwa mshambuliaji Peter Tino aliyefunga bao la kusawazishia dakika za mwishoni na kuipa Taifa Stars nafasi pekee ya kucheza AFCON hadi leo.

Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Ahmed Jongo. Amin.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
20m ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE →
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
18h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
20h ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
21h ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
2d ago
READ MORE →