FT : Simba 2-1 African Lyon

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
6 Oct 2018
FT : Simba 2-1 African Lyon
Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba wamechupa hadi kwenye nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi baada ya kuichapa African Lyon mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa Jumamosi jioni.

Ikicheza kandanda safi la kitabuni, Simba iliandika bao lake la kwanza kupitia kwa Shiza Kichuya kwenye dakika ya 09 akimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Meddie Kagere aliyetumbukiza majaro murua kutoka upande wa kulia.



Kichuya amefungua rasmi akaunti ya mabao msimu huu baada ya kufunga bao hilo.

Si Kichuya pekee aliyefungua akaunti ya mabao, Emmanuel Okwi naye alifunga bao lake la kwanza msimu huu baada ya kuunganisha kwa kichwa krosi ya Mohammed Hussein kwenye dakika ya 48.

Bao la kufutia machozi kwa upande wa African Lyon lilifungwa na Awadh Juma aliyeachia 'fataki' nje kidogo ya 18 na kumshinda mlinda lango namba moja Tanzania, Aishi Manula.

Simba ilitawala mchezo huo kwa muda mwingi lakini bado kukosekana kwa umakini langoni kumeendelea kuwanyima mabao mengi mabingwa hao watetezi.

Ushindi huo umaifanya Simba ifikishe alama 14 na kuchupa mpaka nafasi ya nne kwenye msimamo.

Djuma akosekana

Katika hatua nyingine inaelezwa kuwa uongozi wa Simba umevunja mkataba wa kocha wake Msaidizi Masudi Djuma baada ya kufikia makubaliano.

Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Simba zimebainisha kuwa kocha huyo atalipwa fedha za kuvunja mkataba wake kwa mwaka mmoja uliokuwa umesalia.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
6h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
12h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
15h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’