Uongozi wa Simba kupitia Kaimu Rais wake Salim Abdallah 'Try Again' umevunja ukimya juu ya sintofahamu inayoendelea kati ya kocha Mkuu Patrick Aussems na Msaidizi wake Masudi Djuma.
Try Again amekiri kuwa ni kweli makocha hao hawana maelewano mazuri na wamekuwa wakifanya vikao mbalimbali kuweza kuwasuluhisha bila ya mafanikio.
Amesema hii sio mara ya kwanza Djuma kuwa na mgogoro na kocha Mkuu kwani hata wakati wa Pierre Lechantre tatizo kama hilo lilitokea na walifanikiwa kulimaliza kupitia vikao vyao.
Try Again amesema taarifa rasmi itatolewa na uongozi wa klabu ya Simba juu ya mwafaka wa sakata hilo ili kusuluhisha kwa faida na maslahi mapana ya klabu.
"Ni kweli kumekuwa na matatizo ambayo yamekuwa yakijirudia baina ya Masoud Djuma na benchi la ufundi, haswa kwa makocha wakuu akiwemo Pierre Lechantre aliyeondoka.
"Tumekuwa tukifanya jitihada za kutatua tatizo hilo, siwezi kueleza mengi kwa sasa ila tutakuja na tamko rasmi baadaye", Try Again ameiambia Azam TV.

ADVERTISE HERE