Wachezaji watatu wa Simba Jonas Mkude, Aishi Manula na Shomari Kapombe ambao wako kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', jana walikosa mazoezi ya mwisho ya Simba kuelekea mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara leo dhidi ya African Lyon.
Wakati Bocco akitarajiwa kukosa mchezo wa leo kutokana na kuendelea kutumikia adhabu ya kukosa michezo mitatu baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Mwadui FC, Simba huenda ikawakosa Manula, Mkude na Kapombe pia.
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema ana kikosi kipana hivyo hata kama wachezaji hao watakosekana, hawawezi kutetereka.
TFF ilitoa ruhusa kwa wachezaji hao kwenda kuvitumikia vilabu vyao (kama watahitajika) kisha kurejea kambini.
Bado Simba ina nafasi ya kuwatumia kwenye mchezo wa leo kama Aussems ataona kuna ulazima wa kufanya hivyo.

ADVERTISE HERE