Bado hatma ya kocha msaidizi wa Simba Masudi Djuma kuendelea kubaki Msimbazi iko gizani baada ya kuibuka kwa taarifa kuwa uongozi wa timu hiyo uko mbioni kuvunja mkataba wake.
Kulingana na taarifa iliyoripotiwa na vyombo vya habari, jana Mwekezaji wa klabu ya Simba Mohammed Dewji 'MO' alikutana na Djuma huku kila upande ukigoma kuweka hadharani kilichozungumzwa.
Mapema kabla ya kukutana na MO, Djuma alifanya mazungumzo ya Kaimu Rais wa Simba Salim Abdallah 'Try Again'.
"Ni kweli nimeitwa na Rais (Salim Abdallah), ila kwa upande wangu tuko tayari kupokea uamuzi wowote watakaouchukua, riziki ni popote, haipatikani Simba peke yake", amesema Djuma
"Kiukweli ninashangazwa sana na maneno ambayo yamekuwa yanazungumzwa juu yangu, Mungu ndio anajua."
Jana jioni Djuma alichelewa kwenye mazoezi ya kikosi cha Simba yaliyokuwa yakifanyika kwenye uwanja wa Boko Veterans sababu ya kuchelewa ikielezwa ni kikao hicho alichokuwa akifanya na mabosi wa Simba.
Hata hivyo baada ya kutua mazoezini alishirikiana kikamilifu na kocha Mkuu Patrick Aussems kukiandaa kikosi cha Simba kinachoshuka dimbani kwenye uwanja wa Taifa leo kuikabili African Lyon.

ADVERTISE HERE