Kocha Mkuu wa Simba Mbelgiji, Patrick Aussems anafikiria kufanya uamuzi ndani ya kikosi chake kwa kuanza kuwatumia washambuliaji ambao hawapati nafasi ya kucheza akiwemo Adam Salamba na Mohamed Rashid kwa kile alichokitaja ubutu wa kufunga mabao.
Kauli hiyo aliitoa dakika chache baada ya mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga kumalizika kwa suluhu wikiendi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mchezo ambao kipa wa Yanga Beno Kakolanya aliÂibuka nyota wa mchezo huku Kocha Mwinyi Zahera akikiri kwamba aliwaambia wachezaji wake wapaki basi.
Huo, ni mchezo wa tatu wa ligi unamalizika kwa washamÂbuliaji wake tegemeo walÂiokuwepo kwenye kikosi cha kwanza Emmanuel Okwi na Meddie Kagere kutoka uwanÂjani bila kufunga, mingine ni dhidi ya Ndanda FC na Mbao.
Aussems alisema amesikitishwa na nafasi nne za wazi ambazo washamÂbuliaji wake wamezipata na kushindwa kuzitumia vema kufunga mabao katika mchezo wao na Yanga na hilo limeÂtokana na umakini mdogo wa wachezaji hao, lakini ubora wa Kakolanya.
âUtafikia muda nitaanza kuwatuÂmia washambuliaji ambao hawapati nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza kwa kuwa nimeona wale ambao wapo hawanipi ninachotaka,âalisema Kocha huyo ambaye ana presha kubwa kutokana na gharama ya kikosi chake na malengo aliyopewa na uongozi.
âKwa sababu mimi ninaÂtaka kuona washambuliaji wakifunga mabao kwa faida ya timu na siyo kitu kingine, hilo wazi kama washambuliaji wangu wamecheza mechi tatu za ligi bila ya kufunga bao hakuna sababu ya kuenÂdelea kuwatumia na badala yake ninatakiwa kuwatumia wengine, sawa kipa wa Yanga alikuwa bora kwa nini wao hawakuwa bora kufunga.
âHivyo, nimepanga kuÂwatumia washambuliaji wengine ambao hawapati nafasi za kucheza ili na wao waonyeshe uwezo wa kufunÂga mabao, labda wanaweza kutupa matokeo mazuri,â alisema Aussems.
Mpaka mchezo huo unamalizika, Simba iliongoza kwa umiliki wa mpira ambao ni 62% kwa 38% lakini mashuti ya maana yaliyolenga lango yaliyopigwa na mastraika wa Simba ni 14 wakati Yanga ni matatu.
Championi

ADVERTISE HERE