Matukio yote ya utovu wa nidhamu uwanjani yakemewe bila ubaguzi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Oct 2018
Matukio yote ya utovu wa nidhamu uwanjani yakemewe bila ubaguzi
Tumesikia jana klabu ya Yanga imeandika barua kwa TFF ikitaka kiungo wa Simba James Kotei aadhibiwe baada ya kuonekana akimpiga ngumi ya bega beki wa Yanga Gadiel Michael kwenye mchezo wa watani wa jadi uliopigwa Jumapili iliyopita.

Aidha uongozi wa Yanga umekwenda mbali zaidi kwa kumtaka Kotei aombe radhi kwa tukio lile.

Kimsingi matukio yote yasiyo ya kiungwana kwenye mchezo wa soka hayakubaliki na yafaa yakemewe.

Yanga wamezungumzia tukio alilofanyiwa mchezaji wao lakini hawakuzungumzia matukio ambayo yalifanywa na wachezaji wao dhidi ya wale wa Simba.

Mfano ni tukio la Andrew Vicent kujaribu kumpiga kichwa nahodha msaidizi wa Simba Mohammed Hussin Zimbwe Jr.

Vicent angeweza kupewa kadi nyekundu kama mwamuzi angeamua kuchukua hatua kwani alimuona.

Lakini hakuchukua hatua kwa sababu alifahamu mchezo ule ulikuwa na 'tension' kubwa.

Afisa wa Habari wa Simba Haji Manara amesema uongozi wa timu hiyo haukutaka kuibua matukio hayo kwa kuwa unafahamu yamefanywa na wachezaji wote na yote yanapaswa kukemewa.

Jambo la msingi hapa ni timu zote kukemea matukio ya utovu wa nidhamu yanayofanywa na wachezaji wote na sio kuchagua yale ambayo yananufaisha upande wako.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’