Winga wa Simba, Shiza Kichuya amesema mchezaji anayetambua kupanda na kushuka kwa kiwango chake ni rahisi kufika mbali.
Tangu msimu uanze Kichuya bado hajafanikiwa kufunga bao lolote katika michezo sita waliyocheza hadi sasa.
"Kikubwa ni kufahamu klabu inamtegemea mchezaji kufikia malengo yao, natamani kufungua akaunti yangu ya mabao kwa msimu huu kwani nauona una changamoto ya ushindani mkali.
"Nililobaini ni kuendelea kuongeza umakini wa hali ya juu kuhakikisha ninapopata nafasi nafunga, siwezi kung'ang'ania kuona ligi ngumu kwa sababu tayari wenzangu wameishafunga mabao, hivyo ni kazi kwangu kuondoa gundu hiyo," alisema Kichuya.
Msimu uliopita Kichuya alichezeshwa dakika 90, lakini kwa sasa kocha Aussems anajaribu kumpa nafasi kipindi cha pili, Ibrahim Mohamed 'Mo' ambaye alikosa namba kabisa msimu uliopita.
Mwanaspoti

ADVERTISE HERE