Aussems 'kuwapika' upya Okwi, Kagere

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Oct 2018
Aussems 'kuwapika' upya Okwi, Kagere
Washambuliaji wa Simba, Meddie Kagere na Emmanuel Okwi wamecheza kwa pamoja katika mechi tatu ambapo, hawajafunga bao lolote msimu huu, licha ya kuonekana kuwa miongoni mwa washambuliaji hatari nchini.

Kagere na Okwi wamecheza mechi dhidi ya Ndanda, Mbao na Yanga na kushindwa kufunga hata bao moja huku kila mmoja akiwa na rekodi matata kwenye Ligi Kuu Bara.

Kagere amefunga mabao manne dhidi ya Tanzania Prisons, Mbeya City na Mwadui FC, lakini kwenye mechi zote hizo alicheza sambamba na John Bocco.

Okwi, raia wa Uganda alikuwa Mfungaji Bora msimu uliopita akifunga mabao 20, hajafunga bao lolote mpaka sasa ligi ikielekea mzunguko wa sita.

Lakini, Kocha wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa hajafurahishwa na matokeo hayo dhidi ya Yanga na sasa anajiandaa kufanya kitu ikiwemo kuwapa mbinu mpya mastraika wake ili kuongeza makali.

Pia, amesema kuwa kama mastraika wake wangekuwa makini kwenye mchezo huo, wangepasia nyavuni hata mabao matatu lakini, kukosa kwao umakini na utulivu kumechangia matokeo hayo.

β€œNi kweli, wamecheza mechi tatu bila kufunga si jambo zuri kwa timu, nitabadili mbinu na kuwapa mpya ili kuongeza makali. Nataka kuwaongezea umakini na utulivu pindi wanapopata nafasi za kufunga ili kuleta matokeo mazuri.

β€œKagere anakutana na changamoto kutokana na kasi yake ya kufunga, kila beki anatamani kumkaba na kumzuia asifunge, lakini Okwi anakosa utulivu na kutokujiamini ndio sababu hajafunga mpaka sasa, japo ni mzuri sana,” alisema Aussems.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’