Licha ya kukosekana kwenye mchezo dhidi ya Yanga juzi, beki Mganda Juuko Murshidi na kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima wamerejeshwa kwenye kikosi cha kwanza cha Simba imefahamika.
Niyonzima na Juuko walirejeshwa Simba wiki mbili zilizopita na kupelekwa kikosi cha pili kilichokuwa kikinolewa na kocha Masudi Djuma ili wapate utimamu wa kimchezo.
Kuelekea mchezo wa juzi dhidi ya Yanga, Juuko na Niyonzima walijumuishwa kwenye kikosi cha Simba kilichokuwa kimeweka kambi Kunduchi kujiandaa na mchezo huo.
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems hakuwaingiza moja kwa moja wachezaji hao kwenye mipango yake kwa kuwa hakuwa amewaona na walikosa mazoezi ya maandalizi ya mwanzo wa msimu yaliyofanyika nchini Uturuki.
Niyonzima na Juuko walikosa maandalizi hayo ikielezwa walikuwa na mgogoro na uongozi wa Simba.
Kurejea kwao kunazidi kuimarisha kikosi cha Simba ambacho sasa kimekamilika kila idara.
Niyonzima na Juuko wameitwa kwenye timu zao za Taifa kwa ajili ya michezo ya kusaka tiketi ya kufuzu kwa michuano ya AFCON 2019.

ADVERTISE HERE