Leo saa 11 jioni mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba watashuka kwenye uwanja wa Taifa kuwakabili watani zao Yanga katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara.
Mchezo huo una umuhimu wa kipekee kwa Simba ambayo tayari imepoteza alama tano msimu huu baada ya kupoteza na kutoka sare mchezo mmoja.
Nguvu ya mashabiki inahitaji sana kwenye mchezo wa leo.
Msemaji wa Simba Haji Manara amesema maandalizi kuelekea mchezo huo yamekamilika. Wachezaji wa Simba wameahidi kupambana na kuhakikisha ushindi unapatikana leo.
"Vijana wako tayari kwa mchezo. Tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini tunaamini tutapata matokeo mazuri. Tunawaomba mashabiki mje kwa wingi uwanja wa Taifa kama ilivyo kawaida yetu."
"Sisi ndio timu yenye mashabiki wengi zaidi nchini. Twendeni Taifa kwa wingi tukaiunge mkono timu yetu ili iweze kuibuka na ushindi."

ADVERTISE HERE