Juzi Kocha wa viungo wa Simba Adel Zrane raia wa Tunisia alitoa maelekezo maalum kwa mabeki wa Simba kuhakikisha wanamdhibiti mshambuliaji wa Yanga Heritier Makambo.
Makambo ndio anaonekana kuwa tishio kwenye kikosi cha Yanga na benchi la Ufundi la Simba limewaanda wachezaji wake kikamilifu kumdhibiti.
Zrane alionekana akiwasisitizia mabeki wake namna ya kumdhibiti Makambo katika mazoezi yaliyofanyika juzi Alhamisi kwenye Uwanja wa Boko Veterani.
βMakambo kama mshambuliaji ana wajibu wa kuisaidia Yanga na ni majukumu yake pia, kwa kiwango chake anaweza kuitishia beki ya Simba, hivyo ni lazima kwa mabeki kuchukua tahadhari kwa mchezaji huyu,β alisikika Zrane akiwaambia wachezaji wake.
Simba imeendelea kujifua kujiandaa na machezo huo utakaopigwa uwanja wa Taifa kesho Jumapili Septemba 30 kuanzia saa 11 jioni.
Jana Simba ilijifua kwenye viwanja vya Gymkhana vilivyoko maeneo ya Posta jijini Dar es salaam.

ADVERTISE HERE