Kagere atalipa 'hat-trik' ya Kibaden kesho?

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Sep 2018
Kagere atalipa 'hat-trik' ya Kibaden kesho?
Abdallah Athumani Seif 'King Abdallah Kibadeni Mputa' ndiye mchezaji pekee aliyefunga 'hat trick' katika Kariakoo Derby, akifanya hivyo katika pambano la kihistoria lililopigwa Julai 19, 1977.

Katika pambano hilo lililokuwa la 11 tangu Simba na Yanga kuanza kukutana katika Ligi iliyoasisiwa mwaka 1965, Kibadeni alifunga mabao hayo matatu wakati Simba ikiwafumua watani zo Yanga kwa mabao 6-0.

Kibadeni alifunga mabao yake katika dakika ya 10, 42 na 89, huku mengine yakiwekwa kimiani na Jumanne Hassan 'Masimenti' dk. 60 na 73 na beki wa Yanga, Selemani Sanga alijifunga katika dakika ya 20 ya mchezo huo.

Imefika miaka 41 sasa hakuna nyota yeyote wa klabu hizo aliyeweza kuvunja rekodi hiyo ya Kibadeni, licha ya Simba na Yanga kusajili kila msimu mastaa wa ndani na nje ya Tanzania.

Msimu huu Simba ina washambuliaji wakali ambapo kwenye mchezo huo itawategemea zaidi Meddie Kagere na Emmanuel Okwi baada ya nahodha John Bocco kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Mwadui FC.

Kagere ndiye anapewa nafasi kubwa ya kufunga kwenye mchezo huo kwani amekuwa na mwenendo mzuri wa kuzifumania nyavu tangu kuanza kwa msimu huu.

Tayari ameifungia Simba mabao manne kwenye ligi akiwa miongoni mwa vinara wa kupachika mabao wenye mabao manne msimu huu.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’