Kuna uwezekano mkubwa tiketi za mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga utakaopigwa keshokutwa Jumapili kwenye uwanja wa Taifa zikamalizika mapema.
Mashabiki wameaswa kununua tiketi zao mapema ili kuepuka usumbufu ambao unaweza ukajitokeza hasa kwa wale ambao wanasubiri kununua tiketi zao siku ya mchezo.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Mkurugenzi wa michezo wa TFF Yusuph Singo amesema mauzo ya tiketi yameendelea kwa kasi ambapo mpaka leo mchana tiketi 1300 tayari zilikuwa zimeuzwa.
"Tumejipanga vilivyo kuhakikisha kunakuwepo na usalama wa kutosha, kamera zetu zitafanya kazi ili kusaidia kudhibiti vitendo vyote vya uvunjifu wa amani," amesema.
"Kuna haja kwa upande wa mashabiki wa timu zote mbili kuhakikisha wanajipatia tiketi zao mapema ili kuondokana na usumbufu ambao wanaweza kukutana nao siku husika ya mchezo," alisema Singo.
Vituo ambavyo vitakuwa vinauza tiketi siku ya mchezo ni Uhasibu, Duce pamoja na Hotel ya PR.

ADVERTISE HERE