Mashabiki kupata fursa ya kupima afya zao uwanja wa Taifa Jumapili

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
28 Sep 2018
Mashabiki kupata fursa ya kupima afya zao uwanja wa Taifa Jumapili
Mashabiki watakaojitokeza kushuhudia mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga watapata huduma ya kupimwa magonjwa mbalimbali ili kutambua afya zao.

Wizara ya Afya imeamua kusogeza huduma zake katika mchezo huo kwa sababu unavutia watu mashabiki wengi, hivyo inaamini watawafikia Watanzania wengi kwa urahisi zaidi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Elimu ya Afya kwa Umma, Ama Kasangala amesema kwamba kupitia kampeni yao ya Furahia Kandanda, Lakini Je Unajua Afya Yako? Pima Jitambue Ishi watakuwepo katika maeneo maalum waliyotenga kwa ajili ya watu kwenda kujua afya zao.

Simba na Yanga zina mashabiki wengi, hivyo tumeamua kusogeza huduma zetu jirani, huduma yetu ya kwanza itakua kuchangia damu, kupima kuhusu magonjwa mbalimbali na kutoa elimu ya afya, tutakuwa na sehemu tatu za kutoa huduma hizi ya kwanza itakua upande wa Simba ya pili Yanga na tatu itakaa katikati,” amesema Naibu huyo.

Katika mchezo huo Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu anatarajiwa kumkabidhi kampeni hiyo Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kampeni hiyo iliyozinduliwa mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Maendelea ya Michezo, Dk. Yussuph Singo amesema kwamba ulinzi umeimarishwa zaidi katika mchezo huo, hivyo mashabiki watakaokwenda uwanjani kwa ajili ya kufanya vurugu watadhibitiwa.

“Tumekuwa na vikao zaidi ya vinne vya maandalizi ya mechi ya Jumapili, tunajua ni Derby lakini pia ni mchezo mkubwa kwa vilabu hivi viwili vyenye mashabiki wengi, tumejipanga vizuri na watu wa usalama".

"Nitoe rai kwa wale wenzetu wanaokuja uwanjani kwa ajili ya kufanya fujo, kamera zetu hapa uwanjani (CCTV) zinafanya kazi vizuri sana yoyote atakayefanya vitu viovu tutambaini, hatutarajii tena mambo ya uvunjaji viti na wizi wa koki kutokea,”amesema Mkurugenzi huyo.

Kwa upande wake, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Clifford Ndimbo amesema kwamba tiketi za kushuhududia mtanange huo zitakuwa zinauzwa maeneo ya jirani na uwanja huo.

“Naomba niseme kuelekea mchezo huu hakuna tiketi itakayouzwa uwanja wa Taifa, tumetenga maeneo jirani na Uwanja huu yatakayotumika kuuzia tiketi hizo, maeneo hayo ni, DUCE, Uhasibu (TIA) na wale wanaotokea maeneo ya Temeke na Chang’ombe tiketi zitapatikana Hotel ya PR, niweke wazi kuwa hakuna mtu yeyote atakayekatiza eneo la Uwanja wa taifa bila tiketi,”alisema.

Bin Zubeiry
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
16m ago
READ MORE →
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
3h ago
READ MORE →
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
5h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
8h ago
READ MORE →
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
23h ago
READ MORE →
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE →
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE →
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE →