Mapema leo kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Emmanuel Amunike alingaza majina ya wachezaji 30 wanaounda kikosi cha timu ya Taifa kitakachoingia kambini kujiandaa na michezo miwili ya kusaka tiketi ya fainali za michuano ya AFCON 2019 dhidi ya Cape Verde.
Katika orodha hiyo Simba imetoa wachezaji wanne ambao ni Aishi Manula, Shomari Kapombe, Jonas Mkude na John Bocco.
Wakati wachezaji hao wakiitwa, wengi wameshangazwa na kuachwa kwa kiungo Shiza Kichuya na beki Erasto Nyoni ambao wako katika kiwango bora.
Hata hivyo licha ya kuachwa kwa wachezaji hao, Wachezaji wengine wanne wa kikosi cha Patrick Aussems wameitwa kuzitumikia nchi mbalimbali.
Mshambuliaji kinara wa mabao Meddie Kagere na kiungo Haruna Niyonzima wameitwa timu ya Taifa ya Rwanda wakati Juuko Murshidi na Emmanuel Okwi wameitwa timu ya Taifa ya Uganda.

ADVERTISE HERE