Hakuna mshambuliaji mwenye uhakika wa namba Simba - Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Sep 2018
Hakuna mshambuliaji mwenye uhakika wa namba Simba - Aussems
Licha ya mashabiki mtaani kutambia majina ya Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na John Bocco wakiamini ndio nyota wanaoibeba Simba kwa sasa, lakini Kocha Mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussems amefichua hakuna mwenye uhakika kikosini mpaka sasa.

Mbelgiji huyo alisema, atakuwa akiwatumia au kutowatumia nyota hao ndani ya kikosi cha kwanza kulingana na aina ya pambano wanaloenda kucheza hivyo, hakuna mwenye uhakika wa namba mpaka sasa.

Bocco, aliyeanzia benchi katika pambano na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Mtibwa Sugar kumpokea Okwi kuumia na kutoka dakika ya 65, hatakuwepo kwenye mechi ya watani Jumapili hii na kuwapa mchecheto mashabiki wa Simba.

Nyota huyo amecheza mechi zote tano za Ligi Kuu akibadilishiwa Okwi na Kagere ambaye jijini Mwanza alianzia benchi na timu kulala 1-0 dhidi ya Mbao.

Okwi mwenyewe alikosa mechi za awali dhidi ya Prisons na Mbeya City kabla ya juzi dhidi ya Mwadui kuishia benchi tu.

Nyota hao watatu walicheza kwa mara ya kwanza pamoja mechi ya Ndanda kabla ya baadaye Okwi kutolewa baada ya kuumia mguu, huku Kagere nae alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na Adam Salamba.

Lakini Kocha Aussems alisema hakuna straika mwenye uhakika wa namba katika kikosi chake cha kwanza na kwamba ataendelea kuwatumia ama kutowatumia kwa pamoja katika mchezo mmoja kulingana na mahitaji yake.

β€œKama tunacheza na aina ya timu inayopenda kuzuia kama Ndanda inanilazimu kuwatumia wote watatu, lakini kama tunacheza na timu ambayo inafunguka hata wawili kati ya hao watakaoanza ni sawa,” alisema Aussems.

Simba imeshacheza mechi tano za Ligi Kuu Bara huku, Kagere na Bocco pekee ndio wakiwa wameifungia mabao matano iliyonayo ikishika nafasi ya nne na alama zao 10, tatu pungufu ya vinara Mbao FC iliyocheza mechi sita.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’