Aussems afunguka sababu ya kugomea kambi Zanzibar

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
27 Sep 2018
Aussems afunguka sababu ya kugomea kambi Zanzibar
Kocha Mkuu wa Simba SC, Mbelgiji Patrick Aussems amesema anauchukulia kawaida mchezo dhidi ya Yanga SC na anauona ni sawa na michezo mingine ya Ligi Kuu Tanzania Bara waliocheza awali.

Kuelekea mchezo huo utakayochezwa tarehe 30 siku ya Jumapili, Simba Sc wameendelea na mazoezi yao katika Uwanja wa Boko Veterani, ambao imekuwa sehemu yao mahsusi ya kujifua siku za karibuni.

Akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mazoezi ya jana, Mbelgiji huyo amesema kwamba haoni tofauti ya kufanya mazoezi Dar es Salaam ama nje ya mkoa au nchi, kwa sababu mtanange huo anauchukulia sawa na mingine.

"Nini tofauti ya kuweka kambi hapa na nje ya hapa, kwangu mimi sioni utofauti wowote, mchezo huu ni wakaida kama michezo mingine,"alisema Kocha Aussems ambaye ana matarajio makubwa ya ushindi.

"Najua mchezo huu ni maalum kwa mashabiki wa Yanga na Simba, lakini tumejipanga kushinda, hakuna timu inayoingia uwanjani kwa mategemeo ya kushindwa hata tungekua tunacheza Lipuli au Liverpool, Real Madrid mategemeo yetu ni kushinda".

Kwa kawaida kumekuwa na maandalizi maalumu kwa timu hizi mbili zinapokaribia kukutana katika michezo ya mashindano mbalimbali na mara nyingi kambi huwa nje Dar es Salaam na hata nje ya nchi.

Wakati mahasimu wao Yanga wamekwenda Morogoro, Simba SC ambayo imewahi hadi kwenda Afrika Kusini kwa maandalizi ya mechi hizi safari hii imebaki tu Dar es Salaam.

Na inaelezwa utashi wa uongozi ulikuwa ni kuipeleka timu Zanzibar kama ilivyo kawaida yao, lakini Mwalimu Aussems amekataa akisema anahofia kuwachosha wachezaji.

Wachezaji wote waliosajiliwa na Simba SC msimu huu wamefanya mazoezi jana chini ya Kocha Aussems na Wasaidizi wake, Mrundi Masoud Juma, Mtunisia Adel Zrane kocha wa mazoezi ya nguvu, Muharami Mohammed 'Shilton', kocha wa makipa isipokuwa viungo wa zamani wa Mtibwa Sugar, Hassan Dilunga na Muzamil Yassin ambao ni majeruhi.

Ikumbukwe katika mchezo huyo Simba itamkosa Nahodha wake, mshambuliaji John Bocco ambaye atakuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoonyeshwa kwenye mechi dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga siku ambayo alifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1.

Yanga inashika nafasi ya pili katika Ligi Kuu, ikiwana pointi 12 baada ya kushinda mechi zake zote za mwanzo, nyuma ya Mbao FC yenye pointi 13 za mechi sita, wakati Simba SC yenye pointi 10 za mechi tano ni ya nne, nyuma ya Azam FC yenye pointi 12 za mechi tano

Bin Zubeiry
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
8h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
14h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
17h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’