Baada ya kuthibitika kwa taarifa kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mbwana Samatta atahitaji kukaa nje kutibiwa kwa wiki sita baada ya kuumia, kocha Salum Mayanga amesema kikosi chake kimejiandaa kucheza dhidi ya Benin bila ya uwepo wake.
Samatta amekuwa ndiye mshambuliaji kiongozi katika kikosi cha Stars na kukosekana kwake kutamfanya kocha Mayanga afikirie kubadili mfumo.
Hata hivyo Stars bado ina washambuliaji mahiri wanaoweza kufanya vizuri.
Simon Msuva, Elius Maguri na Ibrahim Ajib ni baadhi ya washambuliaji wanaoweza kuziba pengo la Samatta.
Stars inaondoka leo kuelekea Benin.

ADVERTISE HERE