Kiungo mahiri Hassani Dilunga aliyesajiliwa kutoka klabu ya Mtibwa Sugar bado anaendelea kuuguza jeraha la kifundo cha mguu.
Dilunga tayari amekosa michezo mitatu ya ligi dhidi ya Ndanda FC, Mbao FC na Mwadui huku pia akitarajiwa kuukosa mchezo dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumapili kwenye uwanja wa Taifa.
Tangu atue Simba, Dilunga ameonyesha kiwango cha hali ya juu na kujihakikisha namba kwenye kikosi cha kwanza cha kocha Patrick Aussems kabla ya kukumbwa na majeraha yake.
Hata hivyo kukosekana kwake kwenye mchezo ujao dhidi ya Yanga sio tatizo kwa Simba kwani fundi Mzambia Cleotus Chama amerejea rasmi kikosini baada ya kuwasili kwa ITC yake.

ADVERTISE HERE