Uongozi wa Simba umesema klabu hiyo itabaki jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo dhidi ya Yanga utakaopigwa Jumapili ijayo, Septemba 30 kwenye uwanja wa Taifa.
Awali ilielezwa Simba ingeondoka jana kwenda visiwani Zanzibar kuweka kambi ukiwa ni utaratibu ambao umekuwa ukitumika miaka yote kabla ya mchezo dhidi ya Yanga.
Haji Manara, Mkuu wa Habari wa klabu ya Simba amesema wameamua kuachana na utaratibu huo mwaka huu.
"Lazima tubadilike, Simba Mpya lazma iende kileo zaidi. Hatuhami kambi kwenda Zanzibar wala Comorro.
"Kufanya hivyo ni kuongeza joto unnecessary..mechi hii ina points tatu kama nyingine tofauti yake ni kucharurana tu.
"Kiufundi sijawahi kusikia Madrid akienda Dubai au Miami kujiandaa na El Classico na Barcelona.
"The last game tuliwafunga tukiwa hapa hapa. Na this time tupo hapa hapa jijini.
"Waache waende Moro au Mombasa. Sisi tupo Dar kwa raha zetu," amesema Manara
Yanga iko mkoani Morogoro ambako imeweka kambi kujiandaa na mchezo huo.

ADVERTISE HERE