Winga mahiri wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba, Shiza Kichuya, amewaambia mashabiki wa Yanga wajiandae kisaikolojia kwa sababu anaamini atafunga bao katika mechi dhidi yao itakayopigwa Jumapili.
Kichuya amesema ana bahati ya kufunga mabao wanapokutana na Yanga na msimu huu amejiandaa kuendeleza furaha kwa mashabiki wake.
"Nadhani mnakumbuka nilichofanya siku hii (akiitaja mechi ambayo aliisawazishia timu yake bao katika dakika za lala salama msimu wa 2016/17)," alisema kwa kifupi mchezaji huyo.
Aliongeza kuwa anaamini ushindi walioupata juzi umeamsha morali mpya ndani ya kikosi chao ambacho baadaye mwaka huu kitapeperusha bendera ya Bara katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba ndiyo mwenyeji wa mchezo huo na kwa mujibu wa kanuni mpya za ligi, itabeba mapato yote yatakayopatikana katika mechi hiyo ya kwanza msimu huu.
Hii itakuwa ni mechi ya kwanza kwa Mbelgiji Patrick Aussems ambaye timu yake itashuka uwanjani na ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa bao 1-0 na tayari ina kikombe cha Ngao ya Jamii waliyotwaa baada ya kuifunga Mtibwa Sugar.

ADVERTISE HERE