Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba kimerejea jijini Dar es salaam jana kutoka Shinyanga na leo kinatarajiwa kuelekea visiwani Zanzibar kuweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Yanga.
Meneja wa Simba Abbas Suleiman Alli amesema watakuwa visiwani Zanzibar kwa siku nne kujiandaa na mchezo huo utakaopigwa Septemba 30 kwenye uwanja wa Taifa.
Simba itakuwa mwenyeji wa mchezo huo wa mzunguuko wa kwanza.
Baadhi ya wachezaji ambao waliachwa jijini Dar es salaam Simba ilipokwenda mikoani sambamba na kocha msaidizi Masudi Djuma wamejumuishwa kwenye safari hiyo.

ADVERTISE HERE