Aussems hana hofu na kibarua chake Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Sep 2018
Aussems hana hofu na kibarua chake Simba
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, ameweka wazi kuwa, hana hofu yoyote kama itatokea anataka kutimuliwa kwa kuwa timu nyingi za Afrika, ikiwemo Simba, zimekosa malengo ya muda mrefu kwenye mchezo wa soka.

Kocha huyo aliyechukua mikoba ya Mfaransa, Pierre Lechantre, tayari amekuwa kwenye wakati mgumu kutokana na kuelezwa kutokuwa na maelewano mazuri na msaidizi wake, Mrundi, Masoud Djuma ambaye amemucha Dar katika mechi za mikoani wanazoendelea kucheza, huku pia matokeo yakionekana kutokuwa mazuri Msimbazi.

Kwa mujibuwa Championi Jumatatu, Aussems amesema kuwa hawezi kuwa na hofu ya kutimuliwa kwenye timu hiyo kwa kuwa suala hilo ni kawaida kwa makocha.

β€œNiwe na hofu au niogope kufukuzwa kwa jambo gani labda ambalo linashangaza? Unajua kazi yangu ni kufundisha na walimu suala la kutimuliwa siyo geni, popote linatokea kwa wakati wowote, sasa nini kwangu cha kunifanya niogope?

β€œKiukweli siwezi kuwa na hofu juu ya hilo, naijua vizuri kazi yangu ni ipi kama mwalimu, lakini tatizo limekuwa kubwa kwa sababu klabu nyingi za Afrika zimekosa malengo ya muda mrefu, ndiyo maana unaweza kuona ndani ya kipindi kifupi.

"timu inakuwa na makocha kibao ila imeshindwa kupata matokeo, hivyo ni jambo jema kuangalia malengo kama hayo anayotaka kufanya Mo (Mohamed Dewji),” alisema Aussems.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
10h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
16h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’