Simba haihofii kukosekana Bocco mchezo dhidi ya Yanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Sep 2018
Simba haihofii kukosekana Bocco mchezo dhidi ya Yanga
Jana Simba imepata ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Mwadui Fc kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara uliopigwa uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.

Ushindi huo ulifanikishwa kwa kiasi kikubwa na nahodha wake John Bocco aliyefunga mabao mawili.

Hata hivyo Bocco hakumaliza mchezo huo baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye dakika ya 77.

Bocco alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumpiga kisogoni mlinzi wa Mwadui FC Revocatus Mgunga.

Mgunga alimfanyia madhambi Bocco wakati wakiwania mpira lakini mwamuzi hakuchukua hatua na kumpelekea Bocco ashindwe kujizuia.

Lakini kukosekana kwake kwenye mchezo ujao dhidi ya Yanga sio tatizo kabisa.

Uwepo wa Meddie Kagere, Emmanuel Okwi na Adam Salamba bado ni habari mbaya kwa Yanga ambayo inaonekana kuwa na mapungufu makubwa kwenye safu yake ya ulinzi.

Simba pia itaimarika zaidi baada ya kurejeshwa kikosini kwa Juuko Murshidi na Haruna Niyonzima ambao walikuwa wakijifua chini ya kocha Msaidizi Masudi Djuma aliyebaki jijini Dar es salaam kwa kazi maalum.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’