FT : Mwadui FC 1-3 Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Sep 2018
FT : Mwadui FC 1-3 Simba
Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo wamerejesha furaha Msimbazi baada ya kuifumua Mwadui FC mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara mzunguuko wa sita.

Simba iliuanza mchezo huo kwa kasi kusaka mabao ya mapema lakini ililazimika kusubiri hadi dakika ya 41 kuandika bao la kwanza kupitia kwa nahodha wake John Bocco 'Adebayor' kwa mkwaju wa penati.

Simba ilizawadiwa penati hiyo baada ya Shiza Kichuya kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari.

Simba iliendelea kutawala mchezo huo na ilifanikiwa kuandika bao la pili dakika chache kabla ya filimbi ya mapumziko mfungaji akiwa Bocco tena.

Bocco alimalizia kazi nzuri iliyofanywa na Meddie Kagere aliyewatoka walinzi wa Mwadui Fc kisha kujaza majaro ya chinichini iliyomkuta Bocco akiwa uso kwa uso na nyavu.

Simba iliyonoga kwelikweli leo iliandika bao la tatu kwenye dakika ya 50 mfungaji akiwa Meddie Kagere aliyepiga shuti kali baada ya kumhadaa mlinzi wa Mwadui FC.

Bao pekee la kufutia machozi kwa upande wa Mwadui FC lilifungwa na Charles Ilafya kwenye dakika ya 81.

Bocco alitolewa nje kwa kadi nyekundu kwenye dakika ya 77 baada ya kumpiga ngumi Revocatus Mgunga.

Bocco ataukosa mchezo dhidi ya Yanga utakaopigwa Septemba 30.

Bocco aandika Historia

Mabao mawili aliyofunga kwenye mchezo wa leo yamemfanya John Bocco afikishe jumla ya mabao 100 tangu alipoanza kucheza ligi kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2008/09.




Septemba 24, 2008, Bocco alifunga goli lake la kwanza Ligi Kuu Tanzania wakati Azam FC iliposhinda 2-0 dhidi ya Toto Africa ya Mwanza.

Msimu uliopita 2017/18 ulikuwa wa 10 kwa Bocco akicheza ligi kuu Tanzania bara, katika msimu huo alifunga magoli 14 na kumfanya afikishe jumla ya magoli 98
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’