Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba leo saa kumi jioni wanashuka kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga kuikabili Mwadui FC kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara mzunguuko wa sita.
Simba iliwasili mkoani Shinyanga juzi ikitokea Mwanza ambako ilipoteza mchezo dhidi ya Mbao FC kwa kufungwa bao 1-0.
Baada ya mwenendo usioridhisha kwa michezo yake miwili iliyopita, Simba inahitaji kushinda mchezo wa leo ili kurejesha utulivu.
Licha ya uongozi wa Simba kusema hautachukua maamuzi yoyote kwa kukurupa kutokana na presha ya mashabiki, matokeo tofauti na ushindi kwenye mchezo wa leo yataongeza presha kwa kocha Patrick Aussems ambaye mashabiki wamepoteza imani kwake ingawa ndio kwanza ametimiza mwezi wa pili tangu ajiunge na mabingwa hao.
Mkuu wa Habari wa Simba Haji Manara amesema maandalizi kuelekea mchezo huo yamekamilika, wachezaji wote waliosafiri na timu wako katika hali nzuri na wana matumaini makubwa ya kufanya vizuri leo.
"Tumejifunza kutokana na makosa yetu. Tunawahakikishia mashabiki wetu kuwa tumekuwa tukifanya jitihada kuhakikisha tunarejesha furaha yenu."
"Mpira ni mchezo wa makosa, kila anayefanya kosa anaadhibiwa. Tunaamini bahati itakuwa upande wetu leo," amesema Manara
Michezo yote inayopigwa leo

ADVERTISE HERE