Kocha Mwadui aingia 'mchecheto' kuivaa Simba iliyojeruhiwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Sep 2018
Kocha Mwadui aingia 'mchecheto' kuivaa Simba iliyojeruhiwa
Kocha wa Mwadui, Ally Bizimungu amesema ushindi walioupata Mbao wa bao 1-0 dhidi ya Simba umewaweka katika mazingira magumu wao.

Mwadui na Simba watacheza kesho Jumapili kwenye Uwanja wa CCM Kambarage, lakini Mrundi huyo ameweka wazi ugumu wa mechi hiyo ni kwamba wapinzani wao hawatakubali kupoteza mara ya pili.

Akizungumza mara baada ya mazoezi yao yaliyofanyika uwanja wa Kambarage, Bizimungu alisema kikosi chake kipo vizuri, lakini anachokifanya zaidi ni kuwaandaa wachezaji wake kisaikolojia ili washinde mechi hiyo.

"Baada ya mechi hii tunakwenda ugenini ambako ni kugumu hivyo ni lazima tushinde hii mechi ingawa kupoteza na Mbao kumeongeza ugumu zaidi.

"Naamini tutapambana kupata matokeo mazuri kwani nafasi yetu haiko vizuri, ni vyema tukaanza kushinda mechi za nyumbani halafu ugenini tutafute ushindi au hata sare, japo hatujaipa kipaumbele matokeo ya sare," alisema Bizimungu.

Simba ilitua kimyakimya mkoani Shinyanga jana tayari kwa mchezo huo ambao una umuhimu wa kipekee kwa mabingwa hao wa soka Tanzania Bara.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
6m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
17h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
20h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
21h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’