Try Again awataka mashabiki Simba wawarushie wachezaji fedha timu ikishinda

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Sep 2018
Try Again awataka mashabiki Simba wawarushie wachezaji fedha timu ikishinda
Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again' amewataka mashabiki wa klabu hiyo kuwarushia fedha wachezaji na makocha wanaposhinda kama walivyorusha chupa timu inapofungwa.

Kauli ya kiongozi huyo imekuja baada ya wachezaji na viongozi kurushiwa chupa na mashabiki wa Simba wa Mwanza baada ya kuchapwa bao 1-0 na Mbao jana.

Matokeo hayo yaliamsha hasira kwa mashabiki wengi wa klabu hiyo waliofika kushuhudia mchezo huo na baada ya filimbi ya mwisho ya mwamuzi, Jonesia Rukyaa walianza kuwarushia chupa za maji viongozi, kocha na wachezaji.

Afisa habari wa Simba, Haji Manara aliyekuwa mhanga zaidi wa tukio hilo baada ya kurushiwa chupa nyingi na mashabiki huku wakisikika wakisema kuwa kocha msaidizi Masoud Djuma haondoki ndani ya klabu hiyo.<

Try Again alisema ni jambo baya ambalo mashabiki wa klabu hiyo wamefanya mkoani Mwanza.

"Kitu kibaya wamefanya kwani viongozi wanahangaika kuhakikisha timu inafanya vizuri halafu wao wanakuja na hasira zao na kurusha chupa. Mbona timu ikishinda hawawarushi wachezaji fedha waokote.

"Sio utamaduni, sio uzalendo, sio mchezo wa kiungwana. Watu wanaacha familia zao, kazi zao kwa ajili ya timu, halafu shabiki anaibuka anafanya hivyo, haisaidii timu. Kama wameanzisha utaratibu huo wa kurusha chupa timu ikifungwa basi warushe hela na dhahabu timu ikishinda," alisema Salim β€˜Try Again’.

Mwanaspoti
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
7h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
13h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
16h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’