Licha ya kuanza vizuri katika kikosi cha Simba, kiungo fundi Haruna Niyonzima bado hajafikia matarajio ya wengi kwa kushindwa kuisaidia timu ipasavyo.
Hata hivyo inadaiwa ameshindwa kung'ara vilivyo ndani ya Simba kutokana na mfumo unaotumiwa na kocha, Joseph Omog.
Niyonzima amejiunga na Simba msimu huu lakini amekumbana na wakati mgumu klabuni hapo.
Hata hivyo tathmini inaonyesha kuwa hata Mohammed Ibrahim aliyekuwa akicheza katika nafasi hiyo kabla ya ujio wa Niyonzima, alitoa pasi moja tu ya bao katika mechi tisa za mwanzo za msimu uliopita.
Rekodi zinaonyesha kuwa mfumo wa Omog unatoa fursa kwa mabeki wa pembeni kutengeneza mabao mengi, huku viungo wakihusika zaidi katika kufunga jambo ambalo bado linamsumbua Niyonzima.

ADVERTISE HERE